Leo Ikulu Rais Magufuli alipokutana na timu ya Taifa stars pamoja na mwanandondi, Hassan Mwakinyo ametoa milioni tano kwa aliyekuwa mchezaji wa mpira, Peter Tino ambaye amewahi kuichezea timu ya taifa mwaka 1979 kwa sasa anajihusisha na kuuza duka la vifaa vya michezo akiwa kama mwajiriwa dukani hupo.

Rais alimuita mbele mchezaji huyo mkongwe ambaye alitumia maneno machache kuipongeza timu ya taifa kwa jitihada walizozionesha siku ya jana na kuletea nchi heshima na ushindi mkubwa.

”Mimi ni mwenzenu nasimama kwa niaba ya wachezaji wazangu ambao tulicheza timu hii ya Tanzania mwaka 1979, kwahiyo nawapongeza kwa kuitoa kimasomaso nchi hii ya Tanzania”. amesema Peter Tino.

Aidha Rais Magufuli mbele ya umati alimuhoji anafanya shughuli gani ambapo alisema kwa sasa anauza duka la vifaa vya michezo.

Hivyo papo hapo Rais aliamuru mchezaji huyo mkongwe apewe shilingi milioni 5 za mtaji zimsaidie kuanzisha biashara yake.

Aidha amewapa zawadi ya viwanja kwa kila mchezaji ameomba wizara husika kuwapimia viwanja hivyo huko jijini Dodoma ambapo vitawasaidia hata mara wakishastaafu mchezo huo wa kandanda.

ACT- Wazalendo yawachimba biti viongozi wake Njombe
Video: Tacip yawamulika mafundi majeneza Manzese

Comments

comments