Rais pekee mwanamke Afrika, Ameenah Gurib-Fakim wa Mauritius anatarajia kujiuzulu wiki ijayo kufuatia mgogoro wa masuala ya fedha ambapo anatuhumiwa kutumia kadi ya benki iliyotolewa na taasisi ya misaada na kujinufaisha mwenyewe kwa maelfu ya dola.

Ameenah Gurib-Fakim  anajiuzulu wiki ijayo baada ya sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa visiwa hivyo.

Rais huyo amekanusha kufanya makosa yeyote na kuainisha kwamba amerejesha fedha zilizotamkwa katika sakata hilo.

Aidha Rais Gurib-Fakim anafahamika kuwa mwanasayansi na mwaka 2015 aliteuliwa kuwa Rais wa heshima wa taifa hilo Mauritius.

Waziri Mkuu Pravind Jugnauth aliwaambia waandishi wa habari kuwa Rais wa Jamhuri ya  Mauritius wamekubaliana tarehe atakayo jiuzulu.

 

 

Tillerson asisitiza uwepo wa uhuru wa vyombo vya habari
Wanaharakati watatu wahukumiwa miaka 10 jela