Hatimaye Mfalme wa RnB, R Kelly amefanikisha kupata kiasi cha $100,000 na kuachiwa kwa dhamana, kwa mujibu wa msemaji wa Polisi Kaunti ya Cook nchini Marekani.

Picha zilizonaswa na paparazi usiku, zinamuonesha R Kelly akiwa amevalia jaketi la rangi ya blu akiwa na mwanasheria wake wakitoka nje ya majengo ya ofisi za polisi alikokuwa akishikiliwa.

Juzi, mwanasheria wake aliwaambia waandishi wa habari kuwa mteja wake hivi sasa hana pesa za kutosha kumlipia dhamana, bali anajaribu kuzikusanya kwa nguvu zote ili afanikishe.

Baada ya msako wa fedha wa siku mbili, wa kiasi ambacho wengi walitegemea angekuwa nacho kutokana na ukubwa wake, R Kelly amefanikisha kujitoa nje ya nondo.

Mwimbaji huyo anashtakiwa kwa makosa ya unyanyasaji wa kingono wa wanawake wanne, watatu kati ya hao wakidaiwa kuwa walikuwa wasichana wadogo.

Ijumaa iliyopita, alijisalimisha polisi ambapo alikuwa akikabiliwa na mashtaka 10. Alitakiwa kujidhamini kwa jumla ya $1 milioni, yaani kila muathirika aliwekewa dhamana ya $250,00. Baadaye, Jaji aliamua kuwa atoe asilimia 10 ya kiasi hicho ili atolewe selo, ambayo ni $100,000.

R Kelly na mwanasheria wake wakitoka nje ya jengo la polisi

R Kelly mwenye umri wa miaka 52, amekana kufanya makosa hayo ambayo anadaiwa kuyafanya kwa miongo kadhaa.

Ameingia kwenye mkono wa sheria siku chache baada ya makala maalum ya ‘Surviving R Kelly’ inayoeleza jinsi alivyohusika katika kuwanyanyasa kingono wasichana wadogo kuachiwa rasmi.

Mwanasheria wake emeeleza kuwa ana kazi rahisi ya kufanya katika kesi hiyo kwakuwa mteja wake hana hatia.

Marekani yaeleza ilivyowachapa Al-Shabaab Jumapili
Nigeria: Buhari aongoza matokeo ya awali, wapinzani walia 'faulu'