Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva nchini aliyefanya kazi katika tasnia hiyo kwa muda wa takribani miaka 15, Aboubakar Shabaan Katwila maarufu kama QChilla ametangaza kutoacha kufanya muziki kama ambavyo alitangaza hapo awali kuachana na muziki.

Leo hii amefanya mahojiano na Clouds FM ambapo alienda kuzungumzia sababu ya kuachana na sanaa ya muziki. mrefu ulikwa

Qchillah amesema ilimchukua muda mrefu kufikia maamuzi hayo na anaamini kuwa huu ulikwa wakati sahihi kuachana na muziki.

Aidha Chillah amesema tangu kutangaza kuacha muziki ameona mapenzi ya watanzania yaliyojificha na mara baada ya kushawishiwa vikali ameridhia kutoiacha sanaa ya muziki.

Amesema ”Tangu nimetangaza kuacha muziki nimeona mapenzi ya watanzania nimeona  mahaba yao, mpaka nimejiuliza tatizo sio support ya watanzania labda ni mimi au sikupata msaada niliohitaji ili kufanikisha maendeleo ya kazi yangu” Qchillah.

Hata hivyo Qchief amesema moja ya watu waliomkatisha tamaa kwa kumnyima msaada aliouhitaji ni mtangazaji wa Clouds FM, Bdozen ambaye alikuwa akimtafuta kwa mambo mbalimbali lakini hakuonesha ushirikiano.

Hata hivyo Bdozen amesema endapo Qchillaha atasitisha uamuzi wa kuacha muziki anamuahidi kumsaidia katika kulisongesha kimuziki kwa kumpa mchango wa mawazo na mbinu.

Qchief ameongezea kuwa hakuwa anatafuta kiki kama ambavyo wengi wanadhani au kama ambavyo wamekuwa wakifanya wasanii wengine wa muziki kwa sasa.

 

 

Tanzania yahitaji wawekezaji kwa wingi ili kupata fursa
Moto wazuka wodi ya wazazi, vichanga matatani