Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Q Jay ambaye aliwahi kutamba na kibao cha Sifai imeelezwa kuwa kwa sasa hali yake kiakili haipo sawa.

Rafiki wa karibu wa Q Jay, Makamua amesema kuwa kwa sasa Q Jay yupo Bukoba na amekuwa kama chokaraa kwani amekuwa anaokota makopo na kuongea vitu visivyoeleweka.

Akielezea chanzo hasa cha tatizo hilo, Makamua amesema kuwa ni kutokana na ugumu wa maisha na msongo wa mawazo kutokana na kuachana na familia yake.

Kwa upande mwingine Makamua amewataka Watanzania wamchangie kwa chochote kile ili aweze kupata matibabu ya haraka, kwani Madaktari wamemueleza kuwa anahitaji msaada wa ushauri na nasaha kutoka kwa watalaamu wa Saikolojia.

Makamua amesema kwa sasa jitihada zinazofanyika ni kumsafirisha kutoka Bukoba kuja Dar es salaam kwanza kwa ajili ya matibabu zaidi.

Bondia Mwakinyo asepa na Milioni 7 Bungeni leo
Makosa 8 unayoweza kutiwa ndani kwa saa 24

Comments

comments