Msanii wa BongoFleva Q Chief ameibuka na kujitetea kuwa hana tofauti yeyote ile na Papii Kocha pamoja na Nguza Vicking ila kuna baadhi ya watu ndio wanataka kuwatia ubaya kuhusiana na kuzimiwa MIC akiwa kwenye jukwaa akitumbuiza.

Ameyasema hayo baada ya siku kadhaa kupita baada ya kuzimiwa Mic akiwa stejini kwenye ‘show’ ya kuwakaribisha kwa mara nyingine katika tasnia ya muziki Papii na mzee Nguza kutokana na kupotea kwa miaka mingi machoni mwa mashabiki na wapenda burudani wa dansi.

“Wakati mimi nina ‘perfom’ wimbo wangu wa kwanza katika ‘show’ wa nikilala naota, nilipata baraka zote kutoka kwa MC wa shughuli, Papii na Baba pia. So kwenye kazi unapoona watu wanamuitikio mzuri inabidi ujiongeze kutokana na wao kuonesha mapenzi yao hivyo mimi nimefanya kazi yangu kama vile ninavyofanya sehemu nyingine kwasababu nina nguvu nyingi katika kazi zangu lakini baadae wakati napanda juu nikashangaa kati kati ya wimbo nimezimiwa kipasa sauti ‘MIC,”amesema Q Chief

 

Makunga abwaga manyanga, ajiuzulu
Meek Mill anena gerezani, aeleza kwanini hataki familia imtembelee