Klabu ya Paris Saint-Germain imekanusha taarifa za kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na mshambuliaji kutoka nchini Brazil Neymar, ili akamilishe mpango wake wa kutaka kurejea nchini Hispania, ambapo inadaiwa anawaniwa na klabu za Real Madrid na FC Barcelona.

PSG wamekanusha taarifa hizo, kwa kueleza hakuna ukweli wowote kuhusu jambo hilo, na wanaendelea kushangazwa kuhusu uvumi huo, ambao umewachanganya mashabiki wao waliopo kila kona ya dunia.

Kipindi cha televisheni cha La Porteria kilichorushwa na Chaneli Beteve ya Hispania mwishoni mwa juma lililopita kiliripoti kuwa, uongozi wa PSG umefikia makubaliano ya siri na mshambuliaji huyo, kuhusu kuvunja mkataba wake, ili aweze kuondoka jijini Paris.

Madai ya kipindi hicho yalikwenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa, uongozi wa PSG umemtaka Neymar kuwalipa kiasi cha Pauni milioni 200 kama fidia za kuvunja makataba, na kisha kwenda anapopataka.

PSG wamesisitiza kulivalia njuga suala hilo kisheria, ili kufahamu chaneli ya Beteve iliyoruhusu kipindi cha Porteria kurusha taarifa za uongo.

Neymar anahusishwa kurejea FC Barcelona ili kufanikisha mpango wa kuziba pengo ambalo huenda likaachwa wazi na mshambuliaji Oussmane Dembele, ambaye tayari ameshaomba kuuzwa mwezi Januari, ili hali upande wa Real Madrid wanamuhitaji, ili kuongeza chachu kweye safu yao ya ushambuliaji, kufautia kuondoka kwa Cristiano Ronaldo.

Sadio Mane aongeza morali Liverpool
Tshisekedi ajipa matumaini ya kushinda uchaguzi wa kiti cha urais Kongo DRC

Comments

comments