Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na msajili wa vyama vya siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba amemtaka Maalim Seif Sharif Hamad kufuta kesi zisizo na mashiko walizofungua mahakamani ili kuepukana na hasara ambazo zinaweza kuepukika.

Amesema kuwa si jambo la busara hata kidogo kwa wakati huu ambao nchi ipo katika kipindi cha amani na utulivu kundi la watu likaibuka na kuanza kufungua kesi za kisiasa ambazo kuwepo kwake ni kupoteza muda kwa kundi lililofungua kesi hizo.

Ameyasema hayo Malindi Mjini Unguja alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa lengo la kutoa msimamo wa chama chake juu ya ushiriki wao katika chaguzi ndogo ndogo za wabunge na wawakilishi, katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Jang’ombe utakaofanyika Desemba mwaka huu.

“Hatuwezi kuwaachia fursa ya kushiriki uchaguzi mdogo kwa kisingizio cha mgongano uliopo baina yetu, sisi lengo letu ni kutumikia wananchi hivyo tunaahidi kuwa tutashiriki uchaguzi bila ya wasi wasi wowote,”amesema Prof. Lipumba.

Aidha, amesema kuwa CUF ni sehemu ya vyama vya siasa ambavyo vina haki ya kushiriki uchaguzi huo wa marejeo hivyo ni wazi kuwa hawataacha kushiriki uchaguzi ili kuwapa fursa wananchi kukichagua chama chao ili kuwatumikia.

Hata hivyo, kwa zaidi ya miaka miwili sasa, Chama cha Wananchi (CUF) kipo kwenye mgogoro mkubwa wa kiutawala uliosababishwa na hatua ya Profesa Ibrahimu Lipumba kujiuzulu na baadaye kutengua uamuzi huo.

 

Wanajeshi 45 wahukumiwa kifo
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Agosti 17, 2018