Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa Serikali inaendelea na mchakato wa ndani wa kufanyia marekebisho na kuimarisha maeneo yaliyo mazuri sheria ya ndoa ya mwaka 1971 na kuwasilishwa Bungeni ili kwenda na wakati.

Ameyasema hayo mapema hii leo Bungeni Mjini Dodoma alipokuwa akijibu hoja mbalimbali zinazo ihusu Wizara yake.

“Serikali inaendelea na mchakato huu wa mapendekezo ya marekebisho ya Sheria hii Bungeni ili iweze kuendana na wakati kwa kuondoa upungufu uliopo kwa maslahi mapana ya nchi yetu”,Amesema Prof. Kabudi.

Aidha, amesema kuwa baada ya miaka 20 kupita tangu sheria hiyo ya ndoa itungwe, Serikali kupitia tume ya kurekebisha Sheria iliifanyia mapitio ya sheria hiyo na kubaini maeneo kadhaa yenye udhaifu na hivyo kuhitaji kufanyiwa marekebisho.

Kabudi amebainisha kuwa  Kutokana na maoni hayo ya tume,mwaka 2008 Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria iliandaa waraka  wa baraza la Mawaziri uliokuwa na mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971,hata hivyo desemba 2010 kabla waraka huo kujadiliwa na kuridhiwa na baraza la Mawaziri, mchakato wa mabadiliko ya katiba ya Jamhuri ya Muungano ukaanza na kulilazimu Baraza kusitisha kwa muda mchakato huo.

Hata hivyo, Sheria ya ndoa mwaka 1971 ni matokeo ya mjadala mpana na shirikishi kupitia waraka wa Serikali namba moja wa mwaka 1969.

Video: Waziri Mwakyembe ajibu kwanini alihudhuria 'Press' ya Roma
Mahakama yamfutia Gwajima kesi ya lugha ya matusi dhidi ya Kardinali Pengo