Prezzo ameweka wazi sababu iliyosababisha kutompost aliyekuwa mpenzi wake, Amber Lulu kwenye Instagram alipokuwa akiadhimisha kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa.

Rapa huyo ambaye jana aliitembelea FNL ya East Africa TV alisema kuwa hakuona sababu ya kufanya hivyo kwani sio ishara ya kuonesha kuwa unampenda mtu fulani.

“Sio lazima umpost mtu Instagram ndio wajue unampenda. Kwani birthday ngapi zimepita lakini mama yangu hajanipost?” Prezzo alifunguka, huku akikataa kuzungumzia sababu za kuachana na mrembo huyo.

Katika hatua nyingine, Prezzo alitambulisha wimbo wake mpya ‘Hamsa Mia’ aliomshirikisha Dogo Janja.

Rapa huyo anayejiita ‘Rais/President’ alisema kuwa kufanya wimbo huo ulikuwa mpango wao wa siku nyingi ambao hatimaye umekamilika.

Iangalie hapa:

Bunge lampitisha Xi Jinping kuongoza bila kikomo
Edu Boy amkaribisha Stamina ulingoni wazichape