Takribani watu zaidi ya 100 wamepoteza maisha katika majimbo mawili nchini India baada ya kunywa pombe ya kienyeji.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo vya habari na Polisi, imeelezwa kuwa tukio hilo limetokea katika wilaya ya Haridwar iliyopo jimbo la Uttarkhand, ambapo ni tukio kubwa la kwanza kutokea ndani ya mwaka huu.

Majirani na ndugu wa marehemu wameeleza kwamba watu wengi waliokufa walikuwa wakilalamikia kuumwa matumbo na kushindwa kupumua vizuri.

Aidha, Ofisa mwandamizi wa polisi katika wilaya ya Haridwar, Janmaijai Prabhakar, amesema kwamba tayari wanawashikilia watu wanne wanaohusika na vifo hivyo, na wanaoendelea kupatiwa matibabu ni 18.

Tatizo la vifo vinavyosababishwa na pombe za kienyeji nchini india limekuwa sugu kwa kutokea mara kwa mara katika maeneo mbalimbali kutokana na raia wengi kutokuwa na uwezo wa kumudu gharama za pombe za viwandani.

Hata hivyo, tukio hilo la sasa limeripotiwa kuua watu wengi tokea la mwaka 2011 lililosababisha wati 172 kupoteza maisha katika jimbo   la West Bengal.

 

 

Wananchi Makambako waishukia Halmashauri kuhusu fidia
Zambia yapiga marufuku mifuko ya Plastiki

Comments

comments