Mlango wa timu ya Marines FC ya Rwanda, Nduwayo Baritez huenda akasajiliwa na timu ya Polisi Zanzibar kwa ajili ya kumsajili msimu ujao 2020/21.

Viongozi wa Polisi Zanzibar wanaendelea kufanya mazungumzo na wakala wa mlinda mlango huyo, na imeripotiwa wapo katika hatua nzuri ya kufanikisha lengo la usajili.

Nduwayo ni miongoni mwa wachezaji wanne wapya wa nje ya Zanzibar wanaowaniwa na timu hiyo, ambayo imedhamiria kufanya makubwa katika msimu ujao wa Ligi Kuu visiwani humo.

Mratibu wa Michezo wa Polisi, Kibabu Haji Hassan amesema kuwa hatua hiyo ni moja ya matarajio yao ya kuiongezea nguvu timu yao, kwa lengo la kuirejeshea heshima timu yao ikiwemo kutwaa ubingwa ambao wameupoteza kwa miaka mingi.

“Kwa ajili ya kuiongezea nguvu timu yetu na kujipanga kwa msimu mpya wa ligi tutasajili wachezaji hao ambao mmoja tayari yumo katika mazungumzo,” alisema Kibabu.

“Tunafanya mazungumzo nae pamoja na wakala wake kama ataweza kukubaliana nasi kuja huku na kama mazingira atayapenda tutamsajili,” alisema.

Amesema wachezaji wengine watatu, wanatarajia kuwatoa Bara, wawili washambuliaji na kiungo mmoja. Mbali na Polisi, Baritez pia anawaniwa na Etincelles FC ya Rwanda.

Morisson apigwa "DANADANA" Young Africans
TIA yawatoa hofu wanaoogopa kujiunga kisa hesabu