Uganda wakazi wa Offaka, wilayani Arua wanawatuhumu polisi nchini humo kwa kuwalazimisha kuwanunulia kreti za bia kama namna ya kutoa rushwa ili waweze kuwaachia huru ndugu zao ambao wapo jela kwa kuvunja sheria za nchi.

Baadhi ya wakazi wamesema wamekuwa wakilazimishwa kufanya mambo nje ya sheria kutokana na kuwa na hamu ya kuwatoa ndugu zao waliofungwa jela.

”Hapa , kama polisi wakimkamata mtu, kitu cha kwanza wanachoomba ni kreti za bia kuanzia kreti 5 hadi 6 kabla ya kufikiria kumuachia ndugu yako,” amesema Ms Lilian Andama Lawrence ambaye ni mkazi wa Offaka.

Wakazi hao wameyasema hayo mbele ya wafanyakazi wa Taasisi za Haki ya binadamu (FHRI), Freedom House na ”Judicial Service Commission” (JSC), ambao walitembelea eneo hilo.

Ms Sydey Etima-Ojara, ambaye ni msaidizi na mshauri wa chama cha JSC na Ms Maria Kaddu Busuulwa ambaye Mwenyekiti wa Taasisi ya Haki na sheria wa FHRI wamesema kuwa wanahitaji kuwaelisha wakazi juu ya kukataa kutoa rushwa inayoombwa na polisi hao.

Ameongezea kuwa kufuatia tukio hili kuna uhitaji mkubwa wa kuwasimamia vyema polisi ili kudhibiti vitendo hivyo.

Mr Ronald Sekajja kutoka JSC ametoa ushauri kwa wakazi na kuwataka kuomba risiti pindi wafanyapo malipo kwa wafanyakazi wa Serikali akijumuisha polisi na wanasheria kwani pesa yeyote inayolipwa kwa Serikali ambayo haina risiti hiyo ni rushwa.

Mr Stephen Ilaam, Ofisa wa zamu katika kituo cha polisi cha Ofaka amesema tangu aanze kufanya kazi katika kituo hicho miezi sita iliyopita mambo kama hayo hayajawahi kutokea ila amewahi kusikia yakitokea siku za nyuma.

 

Hispania yakubali kuwapokea wahamiaji kutoka Afrika
Wanafunzi 195 wapata ujauzito Simiyu