Polisi wanawake mkoa wa Arusha kupitia Mtandao wao (TPF NET) wamepongezwa kutokana na utendaji bora wa kazi zao za kila siku hasa katika suala zima la kudumisha nidhamu na kufanya kazi kwa uaminifu.
 
Pongezi hizo zimetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Ramadhani Ng’anzi wakati wa kuhitimisha maazimisho ya Siku 16 za kupinga Ukatili yaliyoanza rasmi Novemba, 25 mwaka huu.
 
Amesem kuwa askari wa kike wamekuwa mstari wa mbele katika kuwahudumia wananchi lakini pia kudumisha nidhamu kwa kiwango cha hali ya juu katika utendaji wao wa kazi.
 
“Natoa pongezi kwa viongozi wenu wa TPF NET kwa kuwasimamia vyema na kuwaweka kwenye mstari mnyoofu na wale ambao walikuwa na dalili za kwenda kinyume na kazi walirudishwa kwenye njia kuu,”Amesema Kamanda Ng’anzi.
 
Aidha, amesema kuwa ubora wao wa utendaji kazi umekuwa kivutio kwa baadhi ya taasisi na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali mkoani hapo ambapo wamekuwa wakifanya kazi pamoja nao hasa katika Madawati ya Kijinsia na Watoto kupitia harakati za kupinga ukatili na unyanyasaji na kuahidi kujenga ofisi kubwa ya Dawati mkoa itakayotoa nafasi ya faragha kwa wateja.
Kwa upande wake, Kaimu Mwenyekiti wa Mtandao wa askari wanawake mkoani humo, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Edith Makweli amesema kuwa, Mtandao huo kupitia Madawati hayo utaendelea kupambana ili kuweza kutokomeza vitendo vya ukatili na unyanyasaji.
   
 
.
Nicki Minaj aapa kumburuza mtangazaji huyu mahakamani
Machali awatupia zigo wanahabari 'Siku hizi hawafuatilii kazi zangu'

Comments

comments