Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma Gilles Muroto amesema hana taarifa za kukamatwa kwa mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Mugaya Tungu ambaye hadi sasa hajulikani alipo.

Awali ilidaiwa kuwa Mugaya Tungu ambaye ni Mwanafunzi wa Mwaka wa pili wa Shahada ya Sayansi Asili alikamatwa na Polisi juzi huku akidaiwa kuwa ndiye aliyepiga picha kuonesha shida ya maji UDOM.

Mkamu ya mkuu wa chuo Prof. Faustine Bee ameomba radhi kwa Jumuiya ya Chuo kutokana na tatizo hilo lililotokea kwa siku 7 mfululizo.

Taarifa ya Ofisi ya Mahusiano ya Umma na Masoko UDOM imemnukuu Prof. Bee akisema tatizo la ukosefu wa maji lilianza Januari 12 hadi 19, 2020 kutokana na kukatika kwa bomba kubwa linalopelekea maji chuoni hapo.

Katibu wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho, Paschal Michael amesema hana taarifa zozote kuhusiana na Mwanafunzi huyo kukamatwa ingawa amekiri kumfahamu.

Rais Magufuli amteua Zungu kuwa Waziri, Simbachawene ajaza nafasi ya Lugola
Makala: Mfahamu Mbwana Samatta, njia zake na ung'aavu wa nyota yake