Jeshi la polisi mkoani Singida limewataka wananchi kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa amani na utulivu kwani litahakikisha usalama unakuwepo nyakati zote katika kipindi cha kampeni hadi siku ya Uchaguzi Novemba 24, 2019.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Sweetbert Njewike, na kudai kuwa Jeshi hilo limejipanga vyema kuhakikisha usalama unakuwa wa uhakika kama ambavyo wamekuwa wakifanya kazi kwa siku zote.

“Polisi tumejipanga kuhakikisha zoezi la uchaguzi linaenda vizuri kuanzia siku ya kwanza ya kampeni itakapoanza Novemba 17 mwaka huu hadi siku ya mwisho ambayo itakuwa ni ya chaguzi hivyo wananchi kuweni na amani na mshiriki zoezi hilo kwa utulivu,” amesema Njewike.

Kamanda Njewike ambaye alikua akisikiliza kero za wananchi wa Kijiji na Kata ya Mitundu kilichopo Itigi Wilayani Manyoni mkoani humo amesema wananchi wanapaswa kutoa ushirikiano ili kuweza kuwabaini wahalifu na kuimarisha usalama.

“Ni lazima kupata ufanisi katika kazi na ili kufanikiwa hivyo nawasihi tushirikiane kukomesha vitendo vya uhalifu maana wahalifu wanaishi katika jamii zetu hivyo tunatakiwa kuwa kitu kimoja katika kulinda usalama wa maeneo tunayoishi,” amefafanua Kamanda.

Awali wananchi hao walimueleza Kamanda Njewike kuwa wana uhaba wa askari katika Kata ya Mitundu, ukosefu wa Jengo la kituo cha polisi lenye kutosheleza mahitaji pamoja na viongozi wa serikali kutofika mara kwa mara kuona maendeleo yao.

Akijibu kero hizo Kmanda Njewike amewahahakikishia wananchi hao kuzifanyia kazi na kitumia nafasi hiyo kumtambulisha Polisi CPL Jackson Mbusiro ambaye atashirikiana nao kwa ukaribu katika masuala ya kiusalama.

Mitihani ya kiswahili kufanyika kimataifa
Video: Fisi wavamia msiba na kujeruhi watu wawili hoi, DC Mjema ashika kaa la moto