Jeshi la polisi Mkoani Mwanza wanafanya uchunguzi kufuatia kifo cha kijana mmoja mwenye umri kati ya miaka 25 hadi 30 ambaye hajajulikana kwa majina aliyefariki dunia kwa kujilusha kwenye ghorofa ya hoteli ya kitalii ya Golden Crest iliyopo barabara Kenyatta jijini hukoo.

Kamanda wa polisi mkoani humo Jumanne Muliro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa kifo hiko kimekuwa na utata mwingi hivyo wanafanya uchunguzi wa kina kwani hakuwa na damu wala majeraha mahali alipoanguka.

Hata hivyo mashahidi walioshuhudia tukio hilo la kijana huyo kujilusha wamesema kuwa walimuona kijana huyo akijilusha toka ghorofa ya nne ya hoteli hiyo.

Moja ya shahidi aliyefahamika kwa jina la Yahya Miraj amesema ni ajabu mtu kujirusha toka ghorofani bila kuwa na jeraha wala kutoka damu.

Meneja wa hoteli hiyo , Peter Henry amekiambia chombo cha habari cha The Citizen kuwa katika daftari la wageni hakukuwa na jina la mtu huyo na wala hawana taarifa yake yeyote na hakuwa mgeni wao kwa siku hiyo.

MAFURIKO JANGWANI: Barabara zafungwa, Maguta yatumika kuvusha watu kwa TSh. 1,000 (+Video)
Spika ahoji serikali kukwama ujenzi wa bandari ya Bagamoyo.

Comments

comments