Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole amesema kuwa hakuna kiongozi yeyote wa kidini aliyezuiliwa kuiongelea Tanzania na kwamba kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake.

Ameyasema hayo wakati akihojiwa na kituo kimoja cha Television, ambapo amesema kuwa hakuna mtu ambaye ametishwa kwa kusema ukweli juu ya jambo fulani ambalo huenda lipo au linatokea Tanzania.

“Hakuna mtu amezuiliwa kuongea ukweli ndani ya nchi ya Tanzania, hakuna mtu ametishwa kwa kusema ukweli na hasa katika uongozi wa awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, anayesema mtu Tanzania kuna mtu kazuiliwa kuzungumza uhuru wake wa maoni nadhani atakuwa na matatizo ila nachofahamu kwamba mtu kuzungumza lugha ya matusi kwa mujibu wa Katiba yetu na sheria zetu ni makosa,”amesema Polepole

Amesisitiza kuwa viongozi wa dini wapo wazi na huru kusema chochote kile kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hata hivyo, Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali Mst. Projest Rwegasira, alitoa onyo na kuwataka viongozi wa jumuiya za kidini kutotumia mahubiri yao ya ibada kwa kufanya uchambuzi wa masuala ya siasa.

Wolper awaumiza roho wapenzi wake wazamani, ajitangazia ndoa
Aliyeongoza Jeshi kumng’oa Mugabe apewa ‘Tonge Nono’