Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda amewajibu watu ambao wamekuwa wakimhoji juu ya kuhitaji nafasi ya Urais 2020 kuwa rais wa sasa John Magufuli ndiye kiongozi ambaye anafaa kwa sasa kuiongoza Tanzania.

Ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Dodoma ambapo amesema wakati fulani kwenye uongozi wake wapinzani waliwahi kusema serikali yao ni dhaifu haina makali hivyo walikuwa wanataka kiongozi mkali na mwenye uthubutu.

“Wakati fulani kuna baadhi ya watu huwa wananiuliza hivi mzee na wewe si ulikuwa unautaka urais nawajibu tu aka huyu huyu ndiye anayefaa, mimi ni miongoni mwa watu wanaomkubali sana JPM.” amesema Pinda

Aidha,mesema kuwa chini ya Rais Magufuli serikali imefanya baadhi ya miradi mikubwa ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa, mradi wa kuzalisha umeme wa Stigler’s Gauge na Serikali kuhamia Dodoma.

Hata hivyo, Mizengo Pinda ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne alikuwa ni miongoni mwa makada waliojitokeza kutaka kupewa nafasi ya kuwania urais wa Uchaguzi Mkuu 2015 ambapo Rais Magufuli aliibuka kinara.

Live: Rais Magufuli akipokea ndege mpya ya Tanzania
Makonda: Tunabishana, JPM yuko madarakani miaka saba..!