Waziri Mkuu wa zamani, Mizengo Pinda ameeleza namna ambavyo wapinzani walikuwa wakimhitaji kiongozi mwenye sifa kama za Rais John Magufuli kwa muda mrefu hususan wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne.

Pinda ambaye alikuwa miongoni mwa waliowania nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2015, alisema kuwa wapinzani walikuwa wanakosoa kuwa uongozi uliokuwepo wakati huo ulikuwa na udhaifu wa kuchukua maamuzi lakini sasa wamepata walichokitaka lakini hawajielewi.

Akizungumza na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) jijini Dodoma, Pinda alisema kuwa hivi sasa anawashangaa wapinzani kwa kugeuka matakwa yao baada ya kumpata Rais Magufuli ambaye ana sifa walizozihitaji. Alisema awali, wapinzani walikuwa wakitoa kauli zilizomuumiza kuwa Serikali ilikuwa dhaifu.

“Wakati ule kauli hii ilikuwa inaniudhi kwa sababu ilikuwa inanilenga mimi. Lakini sasa hivi ambapo Mungu amesikia kilio chao na kuwapa JPM wameanza kulalamika tena, ni jambo la kushangaza,” alisema Pinda.

Mwanasiasa huyo mkogwe alieleza kuwa ingawa aliomba kuwania nafasi ya kugombea urais, yeye anamkubali Rais Magufuli na anaunga mkono kazi anayoifanya ikiwa ni pamoja na uamuzi wa kuhamia Dodoma.

Japan yapata pigo kuporomoka kwa idadi ya watu, watoto
JPM atikisa Afrika ya Kaskazini mpaka Kusini

Comments

comments