Wabunge 35 pamoja na Peter Mollel mzee maarufu kama Pierre Liquid leo wamerejea nchini kutoka Misri ambapo walienda kuishangilia timu ya Taifa Stars kufuatia mchuano wa kwanza AFCON kwenye kundi C walilopangwa dhidi ya Senegal.

Mchezo ambao ulichezwa jana kwenye uwanja wa 30june Stadium, Misri ambapo Taifa Stars iliangukia pua baada ya kufungwa goli mbili bila kwenye mchuano huo wa ufunguzi.

Pierre na wabunge hao wamerudi kimya kimya na kinyonge mara baada ya timu ya taifa kupoteza mechi yao ya kwanza ikiwa lengo kubwa la safari hiyo ilikuwa ni kuipa nguvu timu ya taifa na kuihamasisha ipate ushindi.

Mechi hiyo imezua mijadala mbalimbali na kuwafanya watu maarufu watoe maoni yao juu ya mchezo huo na ushiriki wa wachezaji wa timu ya Taifa.

Nikkiwapili ambae ni msanii wa bongo fleva kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika.

”Wachezaji wa Senegal wana mishahara mikubwa, wanafundishwa na waalimu wakubwa, wametoka ligi kubwa, na wana ma experience (uzoefu) kubwa..kuna mtu wa Barcelona pale , halafu unataka kuilaumu stars hakuna miujiza…ndio tumeanza tukifikisha wachezaji 7 ligi kubwa duniani tutaongea”.

Watu mbalimbali wametoa komenti zao wakiilaumu timu ya taifa kwa mpira walioucheza siku jana.

Aidha, kwenye kundi C Tanzania na Kenya ndio timu ambazo tayari zimefunmgwa magori mawili kwenye michuano iliyofanyika siku ya jana Juni 23, 2019.

 

 

Video: Mazingaombwe ya AJABU zaidi Duniani | Hawa Wamefariki dunia wakionyesha Mazingaombwe yao LIVE
Waziri ahojiwa kwa tuhuma za kupanga kumuua Makamu wa Rais