Muigizaji maarufu wa Uingereza, Idris Elba amefunga pingu za maisha na mchumba wake Sabrina, katika sherehe iliyofanyika kwa siku tatu nchini Morocco.

Katika picha maalum zilizochukuliwa na Jarida la Vogue, wanandoa hao wapya walionekana wakiwa na furaha ndani ya mavazi yaliyosukwa vyema na wanamitindo maarufu. Suti ya Elba ilisukwa na mwanamitindo, Ozwald Boateng na Sabrina alivalishwa na Vera Wang.

Elba mwenye umri wa miaka 46 na Sabrina mwenye umri wa miaka 29 walikula kiapo cha kupendana kwenye shida na raha katika hoteli ya Ksar Char Bang jijini Marrakesh.

Safari ya ndoa hii ilianza Februari mwaka jana baada ya muigizaji huyo wa ‘Good Deeds’ kupiga goti chini na kumuomba Sabrina kuwa mkewe. Alikutana na Sabrina nchini Canada wakati akiandaa filamu ya ‘The Mountain Between Us’ ya mwaka 2017.


Awali, Idris alifunga ndoa na Hanne Norgaard ambaye ni mama mtoto wake wa kike, Isan (17). Mwaka 2017 wawili hao waliachana na safari mpya ya Elba ikaanza na chombo Sabrina.

Ronaldo amfunika Messi, aweka rekodi ya magoli 600
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Aprili 28, 2019

Comments

comments