Mwanamitindo na mfanyabiashara maarufu nchini Kenya ambaye amewahi kushiriki shindano la Big Brother Afrika (BBA) na kuiwakilisha nchi ya Kenya, Alhuda Njoroge maarufu kwa Huddah Monroe amewatahadharisha wafanyabiashara wote wanaouza bidhaa yake feki.

‘Headline maker’ huyo wa mitandao ya kijamii Afrika Mashariki ambaye miaka michache iliyopita aliamua kuanzisha bidhaa zake za urembo ambazo zinafanya vizuri na kupata umaarufu mkubwa pamoja na masoko ndani na nje ya nchi.

Huddah alibaini kuwapo kwa wauzaji feki wa bidhaa zake ambao wanatengeneza bidhaa hizo na kuziuza kwa gharama ya chini hali inayompelekea yeye kupata hasara na kupoteza wateja wake pamoja na jina la ‘brand’ yake.

Huddah alifanya jitihada za kuliwasilisha jambo hilo serikalini washughulike nalo japokuwa serikali haikutekeleza lalamiko hilo kwa wakati, hivyo Huddah siku ya jana aliamua kuingilia kati na kulishughulikia ipasavyo.

Ambapo aliamua kuvaa vazi la kiisalamu la buibui na kuzunguka mtaani kukagua wauzaji wa bidhaa zake za Huddah na kuwabaini wafanyabiashara hao feki.

Kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika.

”Hii ndiyo maana sahihi ya kufanya jambo kimya kimya, jana nimetembelea wafanyabiashara wote mjini… na nimegundua nani anauza bidhaa feki za Huddah, nitarudi tena kwa ajili yenu” ameandika Huddah.

Aidha kumekuwa na tabia ya watu kuharibu biashara za watu wengine kwa kutengeneza bidhaa feki na kuziuza kwa bei chee, hivyo ni vyema Serikali kutoa msaada kwa wafanyaniashara wanaotumia nguvu kubwa kutengeneza jina la kitu na kisha nguvu hiyo kupotezwa na watu wachache wenye ufinyu wa ubunifu wa kuunda na kutengeneza bidhaa zao.

 

 

 

 

Mume wa Amber Rutty aanguka gafla mahakamani
Orodha mpya ya mabilionea Afrika, Mo Dewji ndani, Dangote ashuka kiwango