Jeshi la polisi mkoani Iringa linamshikilia mbunge (chadema) wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa kwa mahojiano zaidi kutokana na matukio ya kiuharifu yanayotokea mkoani kwake.

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa, (RPC) Julius Mjengi amethibitishia kupigiwa simu kuhusiana na kuzagaa kwa taarifa za kukamatwa kwa mbunge Msigwa katika mitandao ya kijamii .

Kamanda huyo amesema kuwa ni kweli hadi majira ya saa8.25 usiku jana Msigwa alikuwa akihojiwa juu ya matukio ya uvunjwaji wa nyumba ya aliyekuwa diwani wa kata ya Mwangata kupitia chadema aliyejiuzulu na kujiunga na CCM pamoja na tukio la kuchomwa moto kwa nyumba aliyokuwa akiishi katibu wa UVCCM Iringa mjini .

“Bado tunaendelea kumhoji na ni kweli amekamatwa tupo naye tunaendelea kumhoji ” amesema Kamanda wa polisi Iringa, Julius Mjengi.

Chama cha SPD chataka kuanza upya mazungumzo na CDU na CSU
Video: Halima Mdee, Bulaya wasema moto ni ule ule, Scorpion atupwa jela miaka saba