Kocha wa Crystal Palace Alan Pardew anaamini kwamba Arsenal wamefanya kosa kubwa kutomsajili kiungo wa klabu hiyo Yohan Cabaye wakati akihama kutoka klabu ya PSG msimu huu wa majira ya joto.
Arsenal walijaribu kumsajili Cabaye mwezi January mwaka 2014, wakati akiwa Newcastle kabla ya kutua PSG ambako kukosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Laurent Blanc, kumemfanya Mfaransa huyo kuamua kurudi kukipiga EPL kwa mara nyingine tena.
Lakini Pardew, kwa upande wake bado anaamini kuwa Cabaye ana uwezo wa kutosha kuichezea Arsenal, na hivyo anajihisi ni mwenye furaha kuweza kumpata kiungo huyo maridadi ambaye hapo awali alifanya naye kazi akiwa Newcastle.
“Nadhani angefanya makubwa sana pale Arsenal, lakini ni lazima tuwe tu wakweli, huyu kijana ana uwezo mkubwa sana katika eneo la kiungo, sidhani kama angeenda Arsenal eti angekosa nafasi katika kikosi cha kwanza, maana kwa kipindi ambacho angekaa klabuni hapo basi angezoeana na wenzake na kufanya mambo makubwa tu”, Pardew aliwaambia waandishi.
“Ni mchezaji wa ajabu sana, tunajisikia ni wenye furaha kubwa kumpata na naweza kusema kuwa ni mchezaji wa kiwango cha Arsenal kabisa huyu. Hivyo sidhani kama Arsene Wenger ama mtu mwingine yeyote pale Arsenal ambaye anaweza kupingana na hilo.
“Tuna mchezaji ambaye angeweza kucheza pale kwao, hivyo hilo ni jambo jema kwetu”.

Mabasi Yaendayo Kasi Kuanza Kazi Leo Dar, Abiria Kupanda Bure
TWIGA STARS YAENDELEA KUJIFUA ZANZIBAR