Papa Francis, amemteua Padre Francis Magalla, kuwa msimamizi wa muda wa jimbo la Mbeya baada ya kifo cha aliyekuwa askofu wa jimbo hilo, Evaristo Chengula hadi hapo atakapo teuliwa Askofu mwingine.

Awali padre Francis Magalla, kabla ya kuteuliwa kukaimu nafasi hiyo, alikuwa Naibu Askofu wajimbo katoliki la Mbeya,nafasi aliyoitumikia baada ya kuteuliwa na Askofu Chengula kuwa Naibu wake tangu alipotangazwa kuwa Askofu wa jimbo la Mbeya baada ya kuteuliwa na Papa Yohane Paulo II .

Aidha,Papa Francis ametoa salamu za pole kwa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) pamoja na mapadre watawa wakike, wakiume na waumini wote wa jimbo la Mbeya kufuatia kifo cha Askofu Chengula aliyefariki Novemba 21, mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.

Akitoa shukurani zake mara baada ya kutangazwa kuwa msimamizi wa Jimbo hilo, Padre Magalla ameshukuru, na kuomba mchakato wa kumteua Askofu wa jimbo hilo uweze kufanyika mapema na kwamba katika wakati wa usimamizi wake atayaenzi yote yaliyofanywa na Askofu Chengula.

 

Mhadhiri alia na rushwa ya Ngono UDSM, amtaka JPM kuingilia kati
Ligi ya mabingwa barani Ulaya: Saba zatangulia 16 bora

Comments

comments