Baraza la Ushauri wa watumiaji wa huduma za usafiri wa nchi kavu na majini, Sumatra limekitaka chama cha wamiliki wa mabasi nchini TABOA na washirika wao kuhakikisha wanasimamia vyema suala la baadhi ya watu wenye tabia ya kugeuza mabasi kuwa sehemu ya mahubiri suala ambalo limekuwa likilalamikiwa kila mara na abiria.

Akizungumza na waandishi na habari, Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri Watumiaji Sumatra, Oscar Kikoyo, amesema kuwa mabasi yatakayo kiuka kanuni hiyo faini zinawanyemelea.

‘Tuna kanuni mpya za mwaka 2017 ya usafiri na hii kanuni ilipigiwa kelele sana, lakini kulingana na kanuni ya 27(b) kipengele cha 3 mabasi si sehemu ya gulio wala mabasi si msikiti wala makanisa kwenda kuhubiri dini kule ndani, amezungumza Kikoyo.

Ameongezea kuwa kufanya biashara pamoja ni miziki na filamu ambazo azikidhi viwango na desturi za Kiafrika, mabasi yanayokiuka  kanuni hiyo wapo hatiani kutozwa faini.

Video: Wanaosema vyuma vimekaza washughulikiwe- JPM
JPM atoa onyo kali kwa wanaofoji takwimu