Hatimaye Baraza la Umoja wa Mataifa limekubali ombi la kuipa fursa ya kipekee Palestina kupeperusha bendera yake katika majengo ya ofisi za Umoja wa Mataifa (UN).

Uamuzi huo ulifikiwa baada ya baraza hilo kupiga kura kufuatia mvutano uliokuwepo wa kuipa Palestina nafasi hiyo. Baraza hilo liliamua kuwa Palestina na Holy See ambayo sio mataifa kamili kwa mujibu wa UN, watapewa nafasi ya kupeperusha bendera zao sambamba na nchi wanachama wa umoja huo.

Hata hivyo, hatua hiyo umekosolewa na Israel ambao ni mahasimu wa Palestina. Israel wameendelea kusisitiza kuwa njia pekee ya kuipa Palestina hadhi ya kuwa taifa huru ni kupitia meza ya mazungumzo ya ana kwa ana na si vinginevyo.

Magufuli Aunga Mkono Wazo Maarufu La Lowassa
Lowassa: CCM Wananizushia, Waandae Maelezo Tukiingia Ikulu