Ni kama kiza kimeingia kwenye Bongo Fleva ambapo kwa mara ya kwanza wasanii wakubwa wamejikuta wakitupiana tuhuma ‘za aibu’ hadharani, wakiuchana-chana uswahiba wao.

Siku moja baada ya Diamond Platinumz kumwaga mboga akidai swahiba wake wa zamani, Ommy Dimpoz alikuwa na tabia za kishoga na kwamba alitaka ‘ampumulie’ lakini alipokataa ikaanza chuki, leo Dimpoz amemwaga mboga kusawazisha matuta yaliyoachwa.

Akifunguka kupitia XXL ya Clouds Fm, Dimpoz amekanusha vikali tuhuma hizo na kueleza kuwa hayo ni maneno ambayo mtu hachaguliwi kuyasema na kwamba anachokifanya ni kutumia busara zaidi ili asijikute ndiye anayeharibu zaidi.

“Ili mradi unajua kabisa wewe ni nani na unafanya nini haiwezi kukuumiza. Na lazima pia uwe mstaarabu kwa sababu unaweza kutumia kitu hasira, ukapaniki ukajikuta wewe ndiye unaenda nje ya msitari kabisa.

“Kwa sababu kama unavyojua, mama zetu hawa wanapenda vijana, wanapenda ujana, wako Instagram na humu. Unaweza ukajikuta umepata hasira umem-DM mama wa mtu, kesho mtu anarudi show anakukuta wewe tena na taulo anaanza ‘kumbe yule ninayempumlia kumbe baba!’” Alisema.

Mkali huyo wa ‘Kajiandae’ alisema kuwa tangu Diamond alipomtolea kashfa hiyo amekuwa akishambuliwa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya watu wanaomuita shoga lakini ameendelea kuwa mvumilivu.

Msanii huyo alieleza kuwa chanzo cha mgogoro wao ni muziki akidai Diamond alikuwa akimbania kumtambulisha kwa wasanii wakubwa kila alipokuwa akimuomba huku akimzunguka kwa baadhi ya mitego yake aliyokuwa ameiweka kupata collabo.

Alidai kuwa hata ujio wa Davido mwaka jana, yeye ndiye aliyekuwa amepanga kufanya nae collabo aliyoambiwa alipie dola 3000, lakini baadae Sallam ambaye ni meneja wa Diamond alimueleza kuwa Diamond ameamua kufanya collabo hiyo na kwamba anailipia dola 5000, hivyo akarudi nyuma.

Aliongeza kuwa kilichochea moto wa bifu kati yao ni yeye kufanya video ya ‘Wanjera’ na Wema Sepetu. Alisema kuwa Diamond ambaye alidai wakati huo alikuwa ameachana naye alikasirishwa na kitendo cha yeye kwenda na Wema bila kumjulisha. Hali iliyozua ugomvi mkubwa kati yao.

Kwa jicho la tatu, kama utakuwa unashawishika na maneno ya Dimpoz, hiyo ilikuwa sababu iliyotibua sababu nyingine za awali kati yao.

Kadhalika, Dimpoz alikanusha kile kilichosemwa na Diamond kuwa anatuma watu wamuombee msamaha, na badala yake ameeleza kuwa Meneja wa Diamond ndiye huwa anamtaka wayamalize ili maisha yaendelee kwa Amani kati yao.

Jana, Diamond Platinumz aliamka na akili zake binafsi na kuamua kuwachana ‘live’ wabaya wake kupitia XXL ya Clouds FM huku akipigia mstari post yake iliyodaiwa kumlenga Ommy Dimpoz akidai ana tabia za ushoga… hali iliyomtoa pangoni Dimpoz.

Giampiero Ventura Asikia Kilio Cha Balotelli
#HapoKale