Mbunge wa jimbo la Geita, Joseph Msukuma amemuomba Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa wachimbaji wote wa madini watumie moja badala ya kujenga masoko mengine kila mkoa.

Msukuma ametoa ombi hilo wakati akitoa salamu kwa Waziri Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi wa hafla ya uzinduzi wa soko la dhahabu lililozinduliwa leo Machi 17, 2019.

Msukuma amesema uwepo wa soko hilo ni ndoto yake ya tangu mwaka 2013 alipozuia ujenzi wa choo katika eneo lenye soko hilo sasa.

Naye Mbunge wa jimbo la Geita mjini, Constantine Kanyasu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, amesema uamuzi wa madiwani kuridhia jengo hilo kuwa soko la dhahabu utaiwezesha halmashauri kuendelea kuongeza mapato yake.

Pia, Mbunge wa jimbo la Busanda, Lorensia Bukwimba amesema pamoja na uwepo wa soko bado wachimbaji wanaomba mazingira rafiki ikiwemo upatikanaji wa umeme wa uhakika.

Wabunge wa mkoa wa Geita wameishukuru Serikali kwa ujenzi wa soko hilo kwa kile walichoeleza kuwa kilikuwa ni kilio cha wachimbaji kwa mrefu, huku wakitaka soko hilo liwe ndilo soko kuu.

Nassari amlilia Ndugai, 'Alihudhuria harusi yangu, bado ana nafasi ya kurejea uamuzi wake'
Agizo la Rais Magufuli latekelezwa, soko la dhahabu lazinduliwa Geita