Mlinda mlango wa klabu ya Wolves inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini England, Carl Ikeme ametajwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria, ambacho kitakabiliwa na mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya barani Afrika za mwaka 2017 dhidi ya Tanzania mnamo septemba 05.

Kocha aliyerithi mikoba ya Stephen Keshi aliyeonyeshwa mlango wa kutokea baada ya kwenda kinyume na mkataba wake, Sunday Oliseh ametaja kikosi cha wachezaji 18 ambacho kitaingia kambini kwa siku kadhaa kabla ya kuja nchini Tanzania kuwania point tatu.

Katika kikosi hicho, Oliseh amemuita mshambuliaji anaecheza soka la kulipwa huko falme za kiarabu Emmanuel Emenike, mshambuliaji wa klabu ya Werder Bremen, Anthony Ujah pamoja na viungo Lukman Haruna na Obiora Nwankwo.

Lakini amewashangaza walio wengi kwa kufanya maamuzi ya kummwaga kiungo wa klabu ya Chelsea John Mikel Obi pamoja na mshambuliaji wa pembeni Victor Moses.

Nahodha na mlinda mlango wa kikosi cha Nigeria, Vincent Enyeama anatarajiwa kuongozana na wenzake katika mpambano huo wa Septemba 05.

Kikosi kamili cha Nigeria ambacho kimetajwa tayari kwa mpambano dhidi ya Tanzania.

Makipa: Vincent Enyeama (Lille, France); Carl Ikeme (Wolverhampton Wanderers, England)

Mabeki: Leon Balogun (FSV Mainz 05, Germany); Kingsley Madu (AS Trencin, Slovakia); Godfrey Oboabona (Rizespor, Turkey); William Troost Ekong (FK Haugesund, Norway); Kenneth Omeruo (Kasimpasa, Turkey)

Viungo: Joel Obi (Torino FC, Italy); Izunna Ernest Uzochukwu (FC Amkar Perm, Russia); Obiora Nwankwo (Coimbra FC, Portugal); Lukman Haruna (Anzhi, Russia); Rabiu Ibrahim (AS Trencin, Slovakia)

Washambuliaji: Ahmed Musa (CSKA Moscow, Russia); Emem Eduok (Esperance, Tunisia); Emmanuel Emenike (Al Ain, UAE); Anthony Ujah (Werder Bremen, Germany); Sylvester Igboun (FC UFA, Russia); Moses Simon (KAA Gent, Belgium)

Zari Ataja Siku Atakayoonesha Sura Ya Mwanae ‘Tiffah’, Azungumgumzia Kumpima DNA
Man Utd Mtegoni Barani Ulaya