Washambuliaji Emmanuel Okwi na Meddie Kagere wa Klabu ya Simba, waamewauzia majonzi JS Saoura wa Algeria baada ya kupachika magoli matatu katika muda wa nyongeza wa kipindi cha kwanza na dakika za awali za kipindi cha pili cha mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika uliomalizika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Okwi ambaye anaitumikia Simba kwa nambari 10 ya kuusaka ushindi, alifanikiwa kuwapenya mabeki wa JS Saoura akiwahadaa na kupata nafasi ya kupachika mpira kimiani, na kuwaandikia goli la kwanza wana Msimbazi dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza.

Mashabiki wa Simba waliokuwa wanashangilia huku wakiwa na wasiwasi, waliibua shangwe la karne baada ya kushuhudia goli hilo la kwanza, hali iliyowasababisha kuimba kwa pamoja msemo maarufu wa Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama wa ‘Yes We Can’.

Kocha Patrick Aussems anastahili pongezi kwa namna alivyofanikisha kuwauza Tai wa Algeria katika kipindi cha kwanza kwa kufanya mabadiliko sahihi. Tai hao walikuwa wanacheza kwa tahadhari ya hali ya juu na kulinda goli lao.

Bila kupiga kope, mshambuliaji Kagere katika dakika ya 51 aliwaliza tena JS Saoura akiwaandikia Simba goli la pili. Kagere hakutulia, akapachika goli lingine la tatu katika dakika ya 67.

Dakika 90 za mchezo wa Ligi ya Klabu Bingwa barani Afrika zimekamilika na Simba wameandika historia ya aina yake ikiongoza kundi lao.

Waumini wamgeuka Imam msikitini, wataka aongoze maandamano
DC Njombe awapa neno Wajasiliamali