Rapa Octopizzo wa Kenya amesema hataki kuwa mbunge au mwanasiasa kwa ujumla, siku moja baada ya kukutana na mbunge kutoka Uganda, Bobi Wine.

Tamko hilo la Octopizzo kupitia mtandao wa Twitter, amelitoa baada ya kuungana na viongozi vijana watano wa kisiasa katika viwanja vya eneo la Kibera nchini Kenya ambapo walifanya mkutano mkubwa Jumatatu ya Oktoba 15.

Mkutano huo uliojaza viwanja hivyo, ulihudhuriwa na wanasiasa machachari akiwemo Mbunge wa Embakasi Mashariki, Babu Owino na Boniface Mwangi.

Octopizzo na Bobi Wine wakisalimia wananchi

Katika tweet hiyo, mkali huyo wa ‘Namba Nane’ alisema kuwa hataki kujihusisha na siasa kwa sababu sio kila mwanasiasa ni kiongozi na pia sio kiongozi ni mwanasiasa. Aliongeza kuwa kama msanii tayari ametumia sanaa yake kuwakilisha matatizo ya jamii.

Amteka mama wa mpenzi wake baada ya mwana kumsaliti
‘Queen’ ya Nicki Minaj yatusua Platinum

Comments

comments