Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama ameunga mkono maandamano yanayofanyika nchini humo yanayoshinikiza kuundwa kwa sera mpya juu ya umiliki silaha.

Barack Obama na mkewe Michelle wameunga mkono maandamano hayo ambayo yalifanywa na wanafunzi siku ya jana kwenye viunga vya jiji la Washington.

“Mimi na mke wangu tumehamasika na kushawishiwa na maandano ya leo (jumapili) yanayofanywa na wanafunzi nchi nzima. Endeleeni kutupigania, Hakuna jambo linaloshindikana kwenye sauti za mamilioni ya watu wanaohitaji mabadiliko,“ameandika Barack Obama kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Miji mingine ambayo wananchi waliandamana ni Boston, New York, Chicago, Houston, Minneapolis, Phoenix, Los Angeles na Oakland, California.

Katika idadi ambayo ilionekana wakati wa enzi za Vita ya Vietnam, na kuwazoa wanaharakati ambao kwa muda mrefu wamevunjwa moyo na mkwamo katika mjadala wa umiliki wa silaha na kuzijumuisha sauti nyingi mpya za vijana.

Telstar 18 wamchukiza David de Gea
Joe Gomez kuikosa Italia