Jeshi la Polisi Mkoni Kigoma limesema kuwa wanamsubiri Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe awasili mkoani hapo, ili kuweza kutoa taarifa rasmi ya kuteketea kwa nyumba yake iliyopo Mwandiga mkoani Kigoma.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui, ambapo amesema kuwa polisi inachelea kutoa ripoti hiyo kwa sababu mwenye nyumba hayuko Kigoma, hivyo hawawezi kujua thamani ya mali ambazo zilikuwepo.

“Bado tunaendelea na uchunguzi wa chanzo cha moto, lakini kwa upande wa kujua gharama mpaka yeye mwenyewe awepo, na nyumba ambayo imeungua ni nyumba ndogo sio nyumba kubwa aliyokuwa anakaa mlinzi,” amesema Kamanda Mtui

Hata hivyo, kwa upande wake mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amewataka wananchi kuwa na subira juu ya ripoti ya tukio hilo, huku akiwashukuru wananchi waliosaidia kuzima moto huo.

Liverpool, Tottenham zashindwa kutamba nyumbani
Jeshi la DRC lawauwa wakimbizi 18