Nyota wa Tenisi nchini Uingereza, Kyle Edmund, amethibitisha kuwa atacheza michuano ya kuwania ubingwa wa Malkia mwezi Juni na itakuwa michuano yake ya kwanza tangu akamate namba moja nchini humo.

Edmund mwenye miaka 23 anayeshika nambari 26 duniani amefanikiwa kuikamata namba moja nchini Uingereza mwezi Machi, akichukua nafasi ya Andy Murray ambaye ameshikilia nafasi hiyo kwa miaka 12.

Katika michuano hiyo ya Malkia Edmund ataungana na bingwa mtetezi, Mhispania Feliciano Lopez pamoja na mshindi wa zamani wa mashindano hayo Rafael Nadal.

Lopez mwenye umri wa miaka 36 alishinda taji hilo 2017 kwa kumpiga Marin Cilic wa Croatia kwa seti 4-6 7-6 (7-2) 7-6 (10-8). Michuano hiyo ya Malkia itaanza Juni 18 hadi 24.

Hata hivyo, Bingwa mara 5 wa michuano hiyo, Muingereza Andy Murray pia anatarajia kushiriki msimu huu ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea michuano ya Wimbledon. Murray mwenye miaka 30 aliumia na kujitoa kwenye michuano ya wazi ya Australia mwezi Januari.

Welayta Dicha kuamua safari ya Young Africans
Video: Serikali yatimiza mambo 5 yatakayo wasaidia Wafugaji