Jeshi la Polisi Mkoani Kagera limethibitisha kumshikilia mlinzi wa Kagera Sugar, Juma Said Nyosso kwa kosa la kumpiga shabiki anayeaminika kuwa ni wa Simba baada ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba uliopigwa mjini Bukoba.

Tukio hilo limetokea baada ya mechi kumalizika na wachezaji wa Kagera Sugar walikuwa wanakwenda katika vyumba vya kubadilishia nguo huku mashabiki wakiwa wanashangilia kwa kutoa maneno makali kitendo ambacho kilimfanya Nyosso akose uvumilivu na kumpiga shabiki huyo.

Aidha, baada ya kupigwa ngumi shabiki huyo alianguka chini na kupoteza fahamu ndipo  Polisi walifika na kumkamata Nyosso na kuondoka naye.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Oromi amesema bado wanaendelea na uchunguzi zaidi wa tukio hilo na wakikamilisha watatoa taarifa kamili.

Video: Halima Mdee, Bulaya wasema moto ni ule ule, Scorpion atupwa jela miaka saba
Dkt. Mollel: Lowassa anaogopa kufukuzwa Chadema