Vituko na mikasa vimetokea pale Karani mmoja nchini Nigeria aliyefukuzwa kazi kudaiwa kuwaeleza wakaguzi wa hesabu kuwa nyoka alikula kiasi cha Naira milioni 36 ambazo ni sawa na dola 100,000 za Kimarekani.

Hatua hiyo imekuja baada ya Karani Philomena Chieshe aliyekuwa akifanyia kazi katika Ofisi ya Bodi ya Mitihani ya Nigeria inayokusanya pesa za mtihani kuwaeleza wakaguzi hao waliobaini upungufu huo wa fedha kwenye idara hiyo.

Bodi hiyo ya mitihani iliiambia BBC kuwa ilitupilia mbali madai hayo na kubainisha kuwa itamchukulia hatua kali za kinidhamu.

Kisa hicho kimezua shutuma na kebehi nyingi katika mitandao ya kijamii nchini Nigeria.

Nayo Tume ya Kupambana na Rushwa nchini Nigeria iliandika ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter uliosema, hauna huruma na wala rushwa huku ikiweka picha ya mwewe akimkanyaga nyoka.

Unga kwenye bahasha wampeleka mke wa Trump Jr hospitali
Simba yaifuata Mwadui FC