Chris Brown anaweza kutupwa jela miezi sita endapo atakutwa na hatia ya kufuga nyani bila kuwa na kibali kutoka idara husika.

Mamlaka ya Wanyama na Samaki ya California imemfungulia kesi mwimbaji huyo wa ‘Loyal’ baada ya kukuta mtoto wa nyani kwenye nyumba yake, walipoenda kufanya ukaguzi Januari 2 mwaka huu.

Chris alijipalia mkaa baada ya kupost kwenye Instagram picha inayomuonesha yeye na binti yake Royalty wakiwa na nyani huyo ambaye amempa jina la ‘Fiji’.

Mkali huyo aliongeza video fupi inayomuonesha akimuuliza maswali Royalty, “huyu ni mwanao…. atakuja kuwa mkubwa kukuzidi, wote mnalingana vichwa.”

Baada ya saa 36, Idara ya Wanyama Pori na Samaki ilipokea taarifa kutoka kwa watu mbalimbali kuhusu tukio hilo na kuagiza kufanyika kwa ukaguzi nyumbani kwa mwanamuziki huyo.

Kwa mujibu wa Kapteni Patrick Foy, walifika nyumbani kwa Chris na kubaini kuwa hakuwepo, lakini waliwakuta wasaidizi wake ambao waliwapa nyani huyo.

Chris ameahidi kushirikiana na vyombo hivyo vya usalama na faili la tukio hilo limepelekwa kwa waendesha mashtaka wa Los Angeles kwa ajili ya hatua zaidi.

Endapo atakutwa na hatia, anaweza kufungwa jela miezi sita.

Magazeti ya Tanzania leo Januari 15, 2018
Rungwe ataka kuijua siri ya kukutana kwa JPM na Lowassa

Comments

comments