Afisa Mhamasishaji wa klabu ya Young Africans Antonio Nugaz amewataka mashabiki wa klabu hiyo wawe na amani, kwani timu yao haiwezi kufungwa na Simba kwenye mchezo wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara (ASFC), ambao utapigwa Julai 12 Uwanja wa Taifa, Dar es salaam.

Baada ya Simba SC kutinga Nusu Fainali kwa kuichapa Azam FC mabao mawili kwa sifuri katika mchezo ambao waliutawala, mashabiki wa timu hiyo wametamba kuwa Young Africans hawatatoka Julai 12.

Nugaz amesema wao wamefurahi kukutana na Simba SC katika hatua hiyo, kwani wana uhakika hawawezi kuwasumbua.

“Siku zote watani wanapokutana mechi zao zinakuwa na utani mwingi, lakini ukiangalia matokeo ya nyuma sisi ni zaidi yao. Tunaamini utakuwa mchezo mzuri wenye ushindani kwa sababu sisi tuliwapasua kwenye mchezo uliopita, nao watataka kulipa kisasi.”

“Lakini bila ya makandokando tuucheze mpira halafu matokeo yapatikane baada ya dakika 90, sisi hatufungwi. Nawaambia mashabiki wa Yanga wasiwe na wasiwasi HATUFUNGWI,” ametamba Nugaz.

Mshindi wa mchezo huo atacheza Fainali dhidi ya mshindi wa Nusu Fainali ya kwanza ya Kombe La Shirikisho Tanzania Bara (ASFC) kati ya Sahare All Stars dhidi ya Namungi FC, Uwanja wa Nelson Mandela mkoani Rukwa mwishoni mwa mwezi huu.

Mchezo wa Nusu Fainali ya kwanza ya ASFC umepangwa kucchezwa Julai 11, Uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga.

Real Madrid yajituliza kileleni
Toto Africans yaomba huruma TFF, TPLB