Benki Kuu ya Tanzania imewato hofu watanzania kuhusiana na maambukizi ya virusi vya Corona kwa njia ya noti za pesa na kwamab noti hizo zimetengenezwa  kwa namna ambayo zinaweza kuzui vimelea kusalia kwenye noti hizo.

Aidha taarifa hiyo imesema maelekezo yanayotolewa na mamlaka zinazoshughulika na Afya kuwa watu waepuke kushikana mikono na kugusana ikiwa ni pamoja na kunawa mikono mara kwa matra

”Tunawashauri wananchi kufanya miamala kwa kutumia njia mbalimbali za malipo kama vile simu za mikononi Internate na Card bila kulazimika kufika kwenye kaunti za benki au ATM kuchukua noti” imesema  taarifa hiyo

Kama ilivyotangazwa na Shirika la Afya Duniani (WHO)  kuwa ugonjwa wa corona ni tishio duniani kote na tayari umeingia nchini tangu machi 16,2020 baada ya mgonjwa wa kwanza kugundulika mkoani Arusha  na wengine wawili mmoja Zanzibar na mwingine Dar es salaam ambapo walitangazwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Aidha wamewasihi wananchi kuwa katika kipindi hiki amabcho taifa liko katika mapambano dhidi ya Covid-19 kuzipuuzia taarifa ambazo zipo mitandaoni ambazo hazina vyanzo vya uhakika zinazohusisha noti zetu na usambazaji wa virusi vya Corona.

 

 

Wagonjwa wa Corona wafikia 6 Tanzania
Ujerumani: Kansela Angela Merkel asisitiza wananchi kubaki majumbani kuzui kuenea kwa Corona

Comments

comments