Klabu ya Norwich City imeweka historia baada ya kuwalaza mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza Manchester City.

Norwich ambayo imepanda daraja na kujiunga na ligi hiyo ilivuruga historia ya Man City ya kucheza mechi 18 bila kushindwa.

Mpira wa Kenny Mclean kutoka katika kona uliwaweka kifua mbele Norwich City baada ya dakika ya 18 kabla ya kuongeza bao katika dakika 30 wakati walipovamia lango la Man City huku mchezaji Todd Cantewel akifunga

Sergio Aguero alipunguza makali ya Norwich kupitia bao la kichwa kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika lakini Teemu Pukki alinyakua mpira wa Nicolas Otamendi mapema katika kipindi cha pili na kuongeza idadi hiyo ya mabao.

Wakati mashambulizi yakiendelea huku Man City wakipambana vilivyo kukataa uharibufu wa historia yao, zikiwa zimesalia dakika mbili, shambulio la Rodri karibu na eneo hatari iliipatia Man City matumaini baada ya kupachika goli lao la pili dhidi ya magoli matatu ya Norwich.

Dakika zikiendelea kuyoyoma, Norwich ilihimili mikiki mikiki ya mashambulizi mazito na kupata ushindi wao wa pili msimu huu.

Norwich ilitoka katika mkia wa jedwali la ligi ya EPL na kupanda hadi nafasi ya 12 huku Man City ikibakia katika nafasi ya pili wakiwa pointi tano nyuma ya Liverpool wanaoongoza lihi hiyo.

Waziri Mkuu awasimamisha kazi watumishi saba
Mambo makubwa manne wasioyapenda wanaume