Benki ya NMB Kanda ya Ziwa Victoria inatarajia kutumia zaidi ya Sh1.2 bilioni kwa uboreshaji mazingira ya utoaji huduma katika sekta ya elimu na afya kwenye mikoa iliyoko ndani ya kanda hiyo
 
Hayo yamesemwa na Kaimu Meneja wa NMB wa Kanda ya Ziwa, Abrahim Agustino ambapo amesema kuwa fedha hizo zitatumika kuweka thamani katika shule za msingi na sekondari na kuboresha miundombinu katika vituo vya afya na Hospitali.
 
Ameyasema hayo wakati akikabidhi meza 62 na viti 62 vyenye thamani ya Shil. 5 milioni katika shule ya sekondari Mugoma wilaya ya Ngara mkoani kagera kupunguza changamoto ya uhaba wa samani shuleni hapo
 
“Samani tunazopeleka shuleni na sehemu za vituo vya afya tunapofikisha vifaa tiba unachochea upatikanaji wa utendaji kazi kupata huduma bora na wanafunzi wanaongeza mahudhurio kwa kuipenda shule yao,”amesema Agustino.
 
Pia amesema kuwa vilikabidhiwa vifaa vya ujenzi wa jengo la utawala na matundu 14 ya vyoo vikiwa na thamani ya Shil 5 milioni katika shule ya sekondari Nyamahanga iliyoko wilayani Biharamulo na kwamba zoenzi hilo la kutoa msaada katika sekta ya elimu ni endelevu kwa mwaka 2018/20.
 
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Ngara Luteni Kanali, Michael Mtenjele ameitaka jamii ya shule ya sekondari Mugoma kutunza samani hizo huku akiwahimiza wanafunzi wa kike kujihadhari na wanaume mafataki wanaowezwasababishia ujauzito.
 
  • Mahakama yatoa uamuzi hati ya kumkamata Lissu, yawaonya wadhamini
 
  • Makonda ajitwisha zigo, sasa kuinusuru Taifa Stars
 
  • Mchungaji ‘afufua maiti’ akioneshwa Live kwenye TV, maswali yazidi majibu

Tanzia: Ruge Mutahaba afariki dunia, JPM amlilia
Rais feki wa Kenya akamatwa, atumia viongozi feki kutapeli