Imeelezwa kuwa klabu ya Nkana ya Zambia imewafungia maisha mashabiki 10 kuhudhuria mechi za timu hiyo kutokana na kuwafanyia fujo wachezaji wake pamoja na benchi la ufundi.

Ikumbukwe mashabiki hao walifanya vurugu kwa kuwarushia mawe wachezaji ikiwemo kuwarushia mawe kwa kutumia manati baada ya kufungwa na Forest Rangers bao 1-0 iliyokuwa ya Ligi Kuu.

Wakati hayo yakijiri nchini Zambia ambapo hali kama hiyo ya vurugu imewahi kutokea katika baadhi ya michezo ya mpira wa miguu ambapo husababisha hadi vyama vya soka vya nchi husika kuzichukulia hatua za kinidhamu timu ambazo zimeshiriki kwa namna moja au nyingine kutokana na ghasia hizo.

Ikumbukwe April, 2016 watu 29 walijeruhiwa baada ya mashabiki wa Al Ahly kutaka kuingia kwa nguvu katika uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria Misri kushuhudia mchezo dhidi ya timu ya Yanga.

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya mambo ya ndani ya Misri ilisema hali hiyo ilitokana na polisi kupuliza hewa ya kutoa machozi kuwatawanya mashabiki wa Ahly walipolazimisha kuingia uwanjani.

katika mchezo huo wa ligi ya mabingwa Afrika Yanga ilitolewa baada ya kufungwa mabao 2-1 na wenyeji wao Al Ahly hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya mchezo wa kwanza Dar es Salaam kufungana bao 1-1.

Video: Tazama hapa wimbo mpya wa Rayvanny 'Chuchumaa'
Amber lulu: Sasa hivi wamekuwa chawa