Mbunge wa Ubungo kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Saed Kubenea amesema kuwa kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kusema kuwa yeye na Mbunge wa Kibamba John Mnyika walitaka kujiunga na CCM, si kweli.

Amesema kuwa hawakuongea vile na Rais bali walikuwa wakizungumza mambo mengine, na Makonda amesema yale ili kuwafurahisha wanachama wa chama cha mapinduzi waliokuwepo kwenye hafla ile.

Aidha, amesema kuwa uchaguzi ujao watahakikisha kuwa wanashinda kwa kishindo hadi serikali inayoongozwa na CCM ishangae.

“Nchi yetu inajenga matabaka, mtu akionekana anaikosoa serikali wanasema huyu mpinzani, akionekana yuko karibu na baadhi ya viongozi wa juu wanasema tunataka kuhamia chama flani, na siku hizi wametupatia jina jipya wanatuita mawakala wa mabeberu,”amesema Kubenea

Kubenea amesema kuwa, wale wanaomuunga mkono Rais Magufuli wengi wao ndio wanaompinga kimya kimya wakishirikiana na wanachama wengine ndani ya chama ambao wanajiandaa kumpinga katika uchaguzi ujao.

Hata hivyo, hayo yamejiri mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, kudai kuwa, amepokea maombi ya wanachama mbalimbali wanaotaka kujiunga na CCM, wakiwemo wabunge wawili wa CHADEMA, Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na wa Kibamba, John Mnyika, wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kisasa la Salenda na barabara unganishi jijini Dar es salaam

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Desemba 21, 2018
Mchomvu awapiga dongo Wasafi... ‘msiwe mnatucheka, mjifunze’