Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally amesema kuwa wadhifa alionao ulikuwa mzigo kwake na ilifikia wakati alitaka kujiuzulu lakini alipewa moyo na mwenyekiti wa chama hicho, Rais Dkt. John Magufuli na watu wake wa karibu.

Ameyasema hayo jana Jumatano Agosti 28, 2019 katika Shule ya Msingi Ubungo Kisiwani katika siku ya pili ya mwendelezo wa ziara yake jimbo la Ubungo.

“Siasa za kiutendaji na usimamizi wa chama kikubwa kama hiki nina umri wa mwaka mmoja, nilikejeliwa sana nikaitwa majina ya uonevu wakati mwingine nampigia mwenyekiti (Magufuli) hii kazi uliyonipa vipi.”amesema Dkt. Bashiru Ally

”Mtoto wangu mkubwa alisema kama angekuwa na hiari kuamua kazi inayonifaa angeniambia baba achana na kazi hii (ya ukatibu mkuu), Magufuli alinishauri maana anajua misukosuko ya uongozi,” amesisitiza Dkt. Bashiru.

Pia, Dkt. Bashiru amewataja mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila kwamba wanatakiwa kurejea shule kusoma somo la uongozi.

RPC atinga mtaani, aondoka na ‘nguruwe’ anayetuhumiwa kulawiti watoto (Video) #OnTheBench
Misri yaja na mikakati ya uwekezaji sekta ya Ngozi nchini