kufuatia ujumbe mzito alioutuma Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akihoji wasanii wa bongo fleva kumtumikia Kafiri, Msanii toka kundi la Weusi, Nikki wa Pili amekanusha tamko hilo na kusema si kweli usemi huo.

Nikki wa pili ameeleza kuwa wao kama wasanii hawana ufahamu wa kuongelea masuala ambayo yanaendelea mahakamani.

“Hapana hatuwezi kumtenga Mhe. Sugu ila kuna jambo moja naweza kusema kwamba hili suala bado lipo kimahakama na tumeona wenyewe wamewaweka Wanasheria, kwa hiyo sisi wasanii bado hatuna ufahamu wa kujua jambo likiwa Mahakamani unaweza kulisema kwa upande gani kwa maana mara nyingi huwa tunaambiwa tusiingilie kazi za Mahakama”, alisisitiza Nikki wa Pili.

Pia ameongezea kuwa wasanii hawana umoja, chama chao hakina nguvu kwa hiyo hata kunapotokea jambo wasanii walitolee sauti kwa pamoja hakuna ‘platform’ ya kushikilia jambo hilo na kujikuta kila msanii yupo peke yake, na kupaza sauti kila mtu peke yake wasanii wengi wanaogopa hilo”, alisema Nikki wa Pili.

Kauli ya Joshua Nassari imemtoka mara baada ya kuwaona wasanii wapo kimya kufuatia kesi inayomkabili Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi anayetuhumiwa kuongea maneno ya uchochezi dhidi ya Rais, pindi alipoendesha mkutano wa hadhara na wananchi Disemba 31, 2017 jijini Mbeya.

Joshua Nassari katika ukurasa wake wa Twitter ameandika hivi.

”Wasanii wa Bongo flava, mmeasahau kabisa harakati za SUGU kupigania muziki, hamtokei, jela hamfikiii kumuona, mmeamua kumtumikia kafiri? Mmesahau alianzisha harakati za kugoma kuimba bure?…

Nikki amebainisha hayo wakati alipokuwa akifanya mahojiano na mwandishi wa habari baada ya Mbunge huyo kutoa lawama zake kwa wasanii katika ukurasa wake wa twitter asubuhi ya leo.’

Jafo aitaka tume kurudisha hadhi ya Walimu
Mourinho atamba kutwaa mataji EPL