Rapa Nikki wa Mbishi amekubaliana na hoja ya rapa na mshindani wake wa hoja, Nikki wa Pili katika hoja kuhusu muziki wa Bongo Fleva na tuzo za kimataifa.

Nikki aka Baba Zohan amezungumzia tweet ya mwana familia huyo wa ‘Weusi’ akidai kuwa muziki wa Bongo Fleva unapaswa kuushukuru muziki wa Nigeria kwa mafanikio yake, ambapo ameeleza kuwa huo ulikuwa ukweli mtupu.

Akiitetea hoja hiyo, Baba Zohan ameeleza kuwa Bongo Fleva ni nakala ya muziki wa Nigeria. Hivyo, amedai wasanii wa Bongo Fleva wanapokuwa wanaitwa kwenye tuzo za kimataifa na wanafikiria kuwa watashinda tuzo hizo wakiwashinda wasanii wa Nigeria ambao wanawanakili ni miujiza.

Nikki wa Pili

“Nikki wa Pili pale alizungumzia kwa maana ya kuwachora kwamba hii art(sanaa) yote tunayojivunia na kutambatamba tumeiga kutoka kwenye nchi za Magharibi. Basi kama hiyo ndiyo sanaa basi tuwashukuru wale,” Nikki aliiambia SnS kwenye mahojiano maalum.

“Wakati mwingine mnaenda kwenye ma-category(vipengele) ambavyo mnashindana nao mnashindwa kuchukua kwa sababu mnaimba kama wao. Hauwezi kuacha kumpa Olamide tuzo yake halafu umpe sijui nani ambaye naye anaimba kama Olamide na yeye ni Mtanzania,” aliongeza.

“Yaani yeye alichokifanya [Nikki] ni kama sarcasm, yaani kama amewakashifu. Yaani ameonesha upumbavu wa wasanii wanaofanya sanaa ya Kitanzania ambao unaimba kama Davido halafu unataka ukakae kwenye category moja na Davido halafu wewe uchukue tuzo. Hiyo ni miujiza…” Alifunguka zaidi.

Alisema kuwa katika tweet hiyo ya Nikki wa Pili, aliona watu waliotoa maoni yao baadhi yao walimshambulia kwakuwa hawakuelewa.

“Nikki labda ulichemka tu pale labda uwasilishaji wako watu hawakuuelewa, lakini… that was right (ile ilikuwa sahihi) nakuunga mkono, ilikuwa ni kweli,”.

Nikki wa Pili na Nikki Mbishi wamekuwa kwenye mgongano wa hoja tangu mwaka 2012/13, wakati Mbishi akiiwakilisha Lunduno na Wa Pili akiiwakilisha River Camp.

Ongezeko la joto lawa tishio Australia
Video: Mhandisi Kilaba aufagilia mfumo wa TTMS

Comments

comments