Uongozi wa jimbo la Ondo nchini Nigeria umetangaza kuwa kesho ni siku ya mapumziko, ambapo Rais Muhammadu Buhari wa nchi hiyo atakua na ziara katika jimbo hilo.

Gavana wa jimbo hilo la Ondo, Arakunrin Akeredolu amemualika Rais Buhari kufanya ziara katika jimbo hilo ambapo pamoja na mambo mengine atazindua miradi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya sherehe za kutimiza miaka mitatu tangu Gavana huyo aingie madarakani.

Akeredolu ametangaza kuwa Wafanyakazi wote katika jimbo hilo kesho hawatakwenda kazini, ili wapate nafasi ya kumpokea Rais Buhari na kushiriki kwenye sherehe hizo.

Sherehe hizo za kutimiza miaka mitatu madarakani kwa Gavana wa jimbo la Ondo, zilianza tarehe 21 mwezi huu na zinatarajiwa kufikia tamati Machi Mosi mwaka huu.

Mwalimu atupwa jela kwa kumsababishia mwanafunzi ulemavu
Tanzania kunufaika na soko la viungo Uswisi

Comments

comments