Msanii maarufu nchini Marekani, Onika Tanya Maraj maarufu kama ‘Nicki Minaj’ ametangaza rasmi kutumbuiza kwenye tamasha la Jeddah World Festival linalotarajiwa kufanyika nchini Saudi Arabia kitendo ambacho kimeibua maswali na mijadala mingi mtandaoni.

Safari hiyo ya Rappa Nicki Minaj nchini Saudi Arabia imezua mjadala mkubwa kutokana na sheria za nchi hiyo ambazo haziruhusu masuala ya buruudani na wanawake kutojisitiri.

Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Julai 18 mwaka huu ambapo baadhi ya mashabiki wameuvamia mtandao wa Tweeter na kuanza kujadili kwamba hakuna mtu yeyote wa taifa hilo ambaye anamtazama vizuri Nicki Minaj mtandaoni.

Hata hivyo, tamasha hilo limewagusa pia wanawake wa taifa hilo na kuihoji Serikali ya nchi hiyo kwamba inakuwaje wanamualika mtu ambaye hajisitiri wakati wao sheria inawalazimisha kuvaa na kuficha maungo yao yote.

Muonekano wa rapa huyo kupitia mitandao ya kijamii umekuwa gumzo katika nchi hiyo ambayo anatarajia kufanya tamasha mubashara huku wengi wakiwa hawakubaliani na Serikali ya nchi hiyo kumruhusu Nicki kutumbuiza katika tamasha hilo.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 6, 2019
Manchester United: Hatutamuongeza mshahara De Gea kama hataki basi

Comments

comments